Mwanahabari wa Kameme TV azungumzia matukio baada ya kupigwa risasi kwenye maandamano

Catherine Wanjeri Kariuki mwanahabari Wa Runinga ya Kameme amezungumza Kwa Mara ya Kwanza hii Leo baada ya kupigwa risasi kwenye Maandamano jumanne wiki hii.
Wanjeri amefichua kuwa huenda maafisa Wa usalama walikuwa wanamlenga kwani kabla ya kupigwa risasi ,maafisa Hao walikuwa wamemfyatulia vitoa machozi.